albania news flag algeria news flag argentina flag bangladesh news flag bolivia news flag brazil news flag burkina faso news flag cameroon news flag chile news flag colombia news flag congo republic news flag côte d'ivoire news flag egypt news flag ethiopia news flag gabon news flag ghana news flag greece news flag india news flag indonesia news flag Iran news flag israel news flag kenya news flag madagascar news flag malaysia news flag Mali news flag mexico news flag morocco news flag Nigeria news flag Pakistan news flag Paraguay news flag Peru news flag Philippines news flag Romania news flag saudi arabia news flag senegal news flag Singapore news flag Slovenia news flag Southafrica news flag Thailand news flag Tunisia news flag Turkey news flag Venezuela news flag
Booking.com
Accounts posts - scroll to load more Post
 Toolbar

Kizaazaa kilizuka bungeni baada ya waziri wa afya Cisily Kariuki kufika mbele ya seneti na kudai kuwa hakuna kaunti imekuwa ikilipia vifaa maalum vya afya almaarufu maseneta wameghadhabishwa na kauli hiyo kwani kulingana na magavana shilingi milioni 200 zimekuwa zikilipia huduma hiyo kutoka kila kaunti

Shughuli za usafiri zimetatizika katika eneo la Bodhei kaunti ya Lamu baada ya daraja la majengo lililoko eneo hilo katika barabara ya Hindi Bargoni Kiunga kusombwa na mafuriko .

Watu wanne wamefariki na wengine wawili kunusurika huko Kitui baada ya gari walilokuwa wameabiri kusombwa na mafuriko katika barabara ya Kitui kuelekea Matinyani. Wakati huo huo familia mia tano kutoka kaunti ndogo za Teso Kusini na Teso Kaskazini zimeathirika na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayozidi kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Anne Karanja mmoja wa wale waliofariki kwenye mkasa wa ndege wa ethiopia mwezi marchi atazikwa hii leo katika eneo la Kabatini,Bahati. Bintiye Caroline Nduta na wanawe Ryan,Kelly na Rubi watazikwa hapo kesho nyumbani kwao Kiangai,Bahati.

Zoezi la upigaji kura kwenye uchaguzi mdogo wa wadi ya Ganda linaendelea vyema licha ya mvua ambayo imeshuhudiwa katika eneo hilo.

Ni afueni kwa mbunge wa Malindi Aisha Jumwa baada ya Mahakama ya Mombasa kumuachilia kwa dhamana ya shillingi millioni moja na mdhamini wa kiasi sawia na hicho au pesa taslimu laki tano. Jumwa alikamatwa baada ya mtu mmoja kupigwa risasi na kuuawa katika eneo la Ganda baada ya mbunge huyo kuzua rabsha katika mkutano uliokuwa ukiendelea.