albania news flag algeria news flag argentina flag bangladesh news flag bolivia news flag brazil news flag burkina faso news flag cameroon news flag chile news flag colombia news flag congo republic news flag côte d'ivoire news flag egypt news flag ethiopia news flag gabon news flag ghana news flag greece news flag india news flag indonesia news flag Iran news flag israel news flag kenya news flag madagascar news flag malaysia news flag Mali news flag mexico news flag morocco news flag Nigeria news flag Pakistan news flag Paraguay news flag Peru news flag Philippines news flag Romania news flag saudi arabia news flag senegal news flag Singapore news flag Slovenia news flag Southafrica news flag Thailand news flag Tunisia news flag Turkey news flag Venezuela news flag
Booking.com
⇠ Users postsPost
 Toolbar

Jaribio la kiongozi wa wengi katika seneti kipchumba murkomen kubuni kamati maalum ya kushughulikia hoja ya kumng’atua gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu imeambulia patupu.

Kwa mara ya kwanza tangu Kenya kupata uhuru baadhi ya wakazi wa vijiji vya Karare na Sagante katika kaunti ya Marsabit wamepokea hati miliki za mashamba yao huku wengi wakiona hati hizi kama njia ya kukwepa umasikini. Na kama Martin Munene anatupa mengi kuhusiana na wenyeji hao ambao sasa wamepata matumaini mapya.

Utata unaohusu uongozi wa Chuo Kikuu Cha Nairobi umechukua mwelekeo tofauti baada ya Profesa Kiama Gitahi ambaye alirejeshwa kazini na mahakama kumtuma likizo Profesa Isaac Mbeche na kumteua Profesa Madara Ogot kuchukua nafasi yake kwa muda. Haya yanajiri huku Profesa Mbeche akisisitiza kuwa hatoondoka akidai kwamba Kiama hana mamlaka ya kuteua makamu naibu chansela. Hapo jana mahakama ya leba ilimrejesha kazini Kiama kama naibu chansela wa chuo hicho hadi pale kesi aliyowasilisha itakaposikizwa na kuamuliwa.

Kwa kile ambacho kimewashangaza wengi, wabunge wa chama cha Jubilee wanaoegemea upande wa Naibu Rais William Ruto wametangaza kuungana na wenzao kuhudhuria mikutano iliyoandaliwa kuipigia debe ripoti ya BBI. Hii leo kiongozi wa wengi katika bunge la seneti kipchumba murkomen amesema wameafikiana kuhudhuria mkutano wa wikendi hii katika kaunti ya mombasa kando na kuandaa mikutano mengine. Nia ikiwa kuwahamasisha wananchi kuhusu yaliyomo ndani ya ripoti hiyo.

Mwanamke mmoja anauguza majeraha katika hospitali ya rufaa ya kisii baada ya kukatwa mkono na shemejiye kufuatia mzozo wa ardhi.

Baada ya runinga ya Citizen kuwaangazia wanafunzi wanaoogelea mto ili kufika shuleni baada ya daraja katika mto Lusumu eneo bunge la mumias mashariki kuvunjika, viongozi wa eneo hilo sasa wanaonekana kuwa njia panda kuhusu ujenzi wa daraja hilo. Baadhi ya waakilishi na viongozi wa eneo hilo waliozuru eneo wamewataka wazazi kushirikiana nao kujenga daraja la muda.